WAKALI HAWA KUKUTANISHWA KATIKA FILAMU MOJA, SIJUI NANI ATAKUWA ZAIDI!!


Imeelezwa kuwa huenda mwaka huu kabla haujaisha wapenzi na wadau wa filamu watapata fursa ya kujionea filamu ambayo inaelezwa itakuwa kutoka kwa wakali wa filamu hapa bongo.


Filamu hiyo itawahusisha wakali wa filamu wa hapa Bongo, Jacob Stephen ‘JB’,Vicent Kigosi ‘Ray’na  King Majuto.

Akizungumzia kuhusu ujio wa filamu hiyo, JB alisema kwenye filamu hiyo yeye na Ray watacheza kama watoto wa King Majuto na kwasasa  wanatafuta mwigizaji wa kike ili kukamirisha mambo yote kwa ukamirifu zaidi.

Panapo uzima tutakuwa na filamu ya pamoja na King Majuto na mwigizaji mmoja wa kike ambaye bado tunamtafuta.mimi na Ray tutakuwa watoto wa King”  alisema JB

Matumaini ya wengi ni kuwa ushirikiano wa mastaa hao utachangia kutoa filamu nzuri, lakini wacha tuendelee kusubiri.Je wewe unadhani nani ataonesha ujuzi zaidi ndani ya filamu hiyo??

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname