HIKI NDICHO ALICHOKISEMA WEMA KUHUSU WIMBO WA 'NTAMPATA WAPI' WA DIAMOND


Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu amesema kuwa, wimbo wa “Ntampata Wapi” ulioimbwa na aliyekuwa mpenzi wake, Diamond Platnumz hakuimbiwa yeye.
Kauli ya mwanadada huyo inakuja baada ya watu wengi kudhani kwamba wimbo huu alitungiwa yeye, lakini staa huyo anabainisha kuwa wakati wimbo huo ulipokuwa unatoka ndio kilikuwa kipindi wametoka kuachana.

Wema alisema kwamba, “Leo nasema rasmi kuwa hii nyimbo hakuniandikia mimi….because nilikuwa naisikia hii nyimbo hata wakati tulipokuwa kwenye uhusiano amekuwa akiimba, akiiandika kwahiyo ilikuwa tu ni moja ya nyimbo zake kama anavyoandika nyimbo zote lakini nadhani tu timing ya kutoka ndio kidogo imekuwa na utata because kaitoa timing ambayo watu wote wakadhani kamuimbia Wema but in real sense noo,” aliongeza Wema.

Wema aliyaweka wazi hayo hivi majuzi alipokuwa jijini Arusha wakati akifanyiwa mahojiano na kituo cha Redio cha Radio 5 cha jijini humo.

Tangaza nasi kwa gharama nafuu sana ya shilingi elfu 10 tu kwa muda wa mwezi mzima, tupigie simu namba 0716514718.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname