KEISHA NA RIYAMA WAAMUA KUPINGA MAUAJI YA ALBINO


Ni takribani wiki mzima sasa tangu staa wa Bongo Movies, Riyama alipoanza kutoa ujumbe mzito, huju akiitaka jamii kuacha na mauaji ya ndugu zetu walemavu wa ngozi.
Msanii huyo amekuwa akisisitiza upendo kwa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi (Albinos) kupitia ukurasa wake pamoja na kwenye mtandao wa Instagram.

Hivi karibuni Riyama aliweka picha akiwa na mwanamziki Keisha ambaye pia ni mlemavu wa ngozi na kuandika kuwa wapo kazini, kitu ambacho mashabiki wake wengi walijiongeza kuwa Riyama na Keisha watakuwa location wakitengeneza filamu ambayo bila shaka itakuwa ikihusiana na maswala ya kupinga mauaji ya ndungu zetu Albino.

Riyama aliandika “Kazini Mungu bariki kazi ya mikono yetu...... ..Sambazaupendo tunawazaa sisi ni watoto wetu mamazetu baba zetu rafiki zetu wao ni kama sisi tuwakumbatie tusiwabague ndugu zetu watanzania wenzetu ….”

Endapo ni kweli watakuwa wanatengeneza filamu hiyo itakuwa ni jambo jema sana. Hii itakuwa sio mara yake ya kwanza kucheza filamu yenye maudhui ya kupinga mauaji ya albino, kwani hapo nyuma alishawahi kucheza filamu ya aina hiyo.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname