NEPAL YATIKISWA TENA NA TETEMEKO LA ARDHI


Ikiwa ni wiki mbili baada ya tetemeko kutokea Nepal, raia wa nchi hiyo wameingiwa na hofu kubwa tena baada ya kukumbwa na tetemeko lingine kubwa.


Itakumbukwa kwamba hapo awali tetemeko la kwanza lililotokea April 25 ambalo lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 8,000 na inasemekana kuwa tetemeko hilo lilianzia katika mji wa Namche Bazar karibu na milima ya Evarest.

Tetemeko hilo limefikia kipimo cha magnitude 7.3 ikilinganishwa na awali ambalo lilifikia kipimo cha 7.8 na tayari watu 29 wameripotiwa kupoteza maisha huku wengine zaidi ya 1000 wakijeruhiwa vibaya.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname