WATOTO WA MIAKA 10 WAVUTA SIGARA KISA NI MITIHANI


Si jambo la kawaida kushuhudia mtoto mwenye umri wa miaka 10 akivuta sigara, lakini kuna hili tukio kutoka nchini Uingereza.


Utafiti huo uliofanyika nchini Uingereza na kuhusisha watoto takribani 1,000 uligundua kuwa 8 kati yao wanavuta sigara asubuhi ya siku ya mtihani.

Utafiti huo uliofanywa mwaka uliopita uligundua pia takriban watoto 37 walikula Chocoleti kama kiamsha kinywa.

Utafiti huo uliofanywa na kampuni ya Opinion Matters ilibaini kuwa asilimia 55% walikuwa wakihofia kuandikisha matokeo duni na kuwa yangeathiri maisha yao ya baadaye.

Uafiti mwengine huru uliofanywa wakati huo huo pia uligundua kuwa asili mia 20% ya wazazi waligundua kuwa watoto wao walishikwa na mhangaiko wakati wa mitihani.

Mzazi mmoja kati ya nane alisema kuwa wakati huo wa kufanya mitihani, watoto walisusia kula kutokana na hofu. Huku 22% wakipoteza usingizi wao mapema kuliko kawaida, 59% walikataa kula wakati wa mitihani huku 74% ya wazazi walikiri kushikwa na mahangaiko sawa na hayo wakiwa wachanga wenyewe.

Hata hivyo mwanasaikolojia wa maswala ya watoto Dakta Claire Halsey anasema kuwa sio jambo la kawaida kwa watoto wadogo hivyo kushikwa na wasiwasi wa mtihani.

''Sio kawaida kwa kweli kuwa mtoto mwenye umri wa miaka 10-11 wanashikwa na hofu katika mitihani yao''.
Naye, Mwenyekiti wa shirika linahusiana na maswala ya watoto John Coe amependekeza kuwa watoto wa umri huo wapewe chakula kwa pamoja ilikupunguza shinikizo la matokeo mema.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname