RAIA WA AFRIKA KUSINI WAENDELEA KUWAKATAA WAGENI


Inakaribia mwezi mmoja tangu kuzuka kwa vurugu nchini Afrika Kusini ambapo wenyeji wan chi hiyo walikuwa wakiwafukuza wageni wa mataifa mengine.


Hali hiyo imeibuka tena baada ya wenyeji kuanzisha operesheni ya kuwafukuza raia wa mataifa mengine ya Afrika kufuatia vurumai za kibaguzi zilizoibuka dhidi ya wageni katika taifa hilo hivi majuzi.

Taarifa zinasema kuwa zaidi ya wageni 400 kutoka Msumbiji walikuwa katika kundi la kwanza kufukuzwa.

Afrika Kusini imechukua hatua hiyo baada ya vurumai ya kibaguzi dhidi ya wageni iliyopelekea watu saba raia wa kigeni kuuawa na wenyeji waliokuwa wakilalama kuwa wamechukua nafasi zao za kazi.

Mapigano hayo ya kibaguzi yalitibuka katika miji ya Durban na Johannesburg pale wenyeji walipoanza kuwavamia wageni pamoja na kuwapora mali yao.

Serikali ya Msumbiji imeshangazwa na hatua hiyo ya kuwaondoa raia wake kwa nguvu huku waziri wake wa maswala ya kigeni Oldemiro Baloi akisema alikuwa anatarajia kufanya mazungumzo na mwenzake wa Afrika Kusini.

Waziri huyo alisema haelewi kwa nini raia wa Msumbiji wanakamatwa na kuondolewa nchini humo kwa nguvu ilhali swala hilo lilikuwa linashughulikiwa baina ya serikali hizo mbili.

Operesheni hiyo ya kuwakamata wageni imekuwa ikiendeshwa majira ya alfajiri hasa katika mitaa duni ya miji ya Durban na Johannesburg.

Hata hivyo, wanaharakati wa haki za kibinadamu walikwenda mahakamani kupinga operesheni Fiela wakisema inahalalisha vita vya kibaguzi vilivyo sababisha vifo vya watu saba wengi wao wakiwa raia wa mataifa ya Afrika.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname