Tatizo la uhaba wa wataalam wa afya wakiwemo madaktari ni moja ya tatizo linaloyakabili mataifa mengi ya Afrika na Marekani Kusini , jambo linalowalazimu madaktari na wauguzi kufanya kazi ya ziada ilikuwatunza wagonjwa.
Imekuwa ni kawaida sana kumsikia daktari anayehudumu katika hospitali ya umma ndiye yuleyule anayekimbia kumhudumia mgonjwa katika hospital ya kibinafsi iliapate pesa za ziada.
Tumekuwa tukisikia taarifa mbalimbali kuhusu madaktari kufanya makosa ndani ya chumba cha upasuaji na hata mara nyingine katika vyumba vya wagonjwa mahututi kwa sababu ya uchovu.
Huko nchini Mexico wagonjwa na jamaa zao wameanzisha kampeini ya kuwatetea wanafunzi wanaojifunza kazi. Ambao wao waliamua kuwapiga picha madaktari wakisinzia na kuzichapisha katika mitandao ya kijamii.
Daktari akiwa kasinzia kazini |
Watu waliochangia mjadala huo katika mitandao ya kijamii walidai kuwa madaktari wakuu wamekwenda kulala na kuwaachia wanafunzi wao kazi nyingi.
Huyu daktari naye hana habari kabisa |
Mbali na hayo, wengi waliwashtumu madaktari waliohitimu wakisema kuwa wanawatelekeza wagonjwa wao kufuatia kuimarika maradufu kwa mishahara yao.
No comments:
Post a Comment