UKITAKA KWENDA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA LAZIMA UJITATHIMINI KWANZA MAVAZI YAKO!!


Kwenye magazeti ya leo moja ya habari kubwa kupitia Gazeti la Mwananchi ni ile habari kutoka Mbeya ambayo inahusu kupiga marufuku baadhi ya mavazi katika hospitali ya Rufaa ambayo iko kwenye Mkoa huo.

Hospitali hiyo ya Rufaa Mbeya imechapisha mabango kwenye milango mikubwa ya kuingia hospitalini hapo ambayo yameandikwa hivi “Ni marufuku kwa mwanaume yoyote kuingia hospitalini hapa akiwa amevaa suruali ya mlegezo,kaptula fupi maarufu kama vipensi na wale waliosuka nywele pia wanaovaa bangili nyingi mkononi na heleni’




Mbali na bango hilo pia bango linalowahusu wanawake limeandikwa hivi “Wanawake wote watakaokuwa wamevaa suruali za kubana, sketi fupi maarufu kama vimini na nguo zenye mipasuo mikubwa inayoacha wazi mabega na vifua wazi pamoja na blauzi zinazoacha vitovu nje hawataruhusiwa kuingia Hospitali hapa kupatiwa huduma yoyote’

Hata hivyo, Ofisa uhusiano wa hospitali hiyo Alinanuswe Mwansasu amesema maelekezo hayo yanawalenga zaidi wafanyakazi wa hospitali hiyo na ndugu wa wagonjwa waliolazwa na wanaowaleta kupata matibabu.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname