65 WAPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA KIPINDUPINDU KENYA


Ugonjwa wa kipindupindu umeendelea kusababisha vifo nchini Kenya ambapo hadi sasa watu 65 wamepoteza maisha.


Kwa mujibu wa Wizara ya Afya nchini Kenya, watu 65 kati ya 326 waliohofiwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu wamepoteza maisha hadi kufikia hivi sasa.

Aidha, taarifa zinasema kuwa, idadi ya wagonjwa walioambukizwa kipindupindu nchini humo imefikia 3,235.

Pamoja na hayo Wizara ya Afya imebainisha kwamba maambukizi hayo yamechangiwa na janga la uhaba wa maji linalolikumba baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Sambamba na hayo pia maafa ya mafuriko yaliyozuka nchini Kenya nayo yamepelekea kuenea kwa ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname