VIONGOZI WAPEWA AGIZO KUHUSU TATIZO LA FISTULA
Leo ni Mei,23, 2015 ambayo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza fistula, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewasihi viongozi wa dunia kujituma zaidi ili kutokomeza janga hili.
Katika taarifa yake, Bwana Ban amesema kila nchi inayokumbwa na tatizo hilo inapaswa kuunda mkakati jumuishi wa kitaifa, ambao utalenga kutokomeza fistula katika kipindi cha kizazi kimoja.
Aidha , ameiomba jamii ya kimataifa kuongeza misaada yake kwa nchi zenye mahitaji zaidi.
Hata hivyo, kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu UNFPA, Babatunde Osotimehin, amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana, mathalan kwa wanawake 47,000 waliofanyiwa upasuaji wa kuponesha fistula, bado juhudi zinahitajika ili kupeleka huduma za afya za uzazi katika jamii duniani kote, kwani bado visa 50,000 hadi 100,000 vya fistula vinatokea kila mwaka.
Shukrani za dhati kwa kutembelea habarimkusanyiko.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment