CCM YAWEKA WAZI RATIBA YA MCHAKATO WA URAIS


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
 Moja ya habari kubwa za leo Jumatatu ya Mei, 25, 2015 katika magazeti mbalimbali hapa nchini ni ile ya kuhusu mbio za kuwania urais na nafasi nyingine kupitia CCM kutangazwa rasmi baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kutoa ratiba, huku ikibainisha kuwa mgombea urais wa chama hicho tawala atajulikana Julai 12, siku mbili baada ya yule wa Zanzibar kufahamika.


Katika taarifa hiyo Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema “Sasa ni ‘ruksa’ kwa wanaotafuta uteuzi wa kupeperusha bendera ya chama katika nafasi za urais, ubunge, udiwani na uwakilishi kuchukua fomu kwa tarehe zilizopangwa,”

Wanaotaka kuwania urais wataanza kuchukua fomu kuanzia Juni 3 hadi Julai 2.

Aidha, Nape alisema Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM ambao ndiyo wenye jukumu la kuchagua mgombea urais wa chama hicho, utafanyika kwa siku mbili kuanzia Julai 11 hadi 12. Alisema mgombea urais wa Zanzibar, atapitishwa na NEC Julai 10.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname