MAKAMU WA RAIS BURUNDI NAYE AMPINGA NKURUNZINZA


Makamu wa Rais Burundi Gervais Rufikiri
Hivi karibuni kulikuwa na stori kuhusu kupingwa kwa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza jambo ambalo lilisababisha machafuko nchini humo sambamba na vifo vya watu.

Sasa taarifa mpya leo ni kutoka katika taifa hilo ambapo makamu wa rais Gervais Rufikiri ametangaza naye kumpinga Rais Pierre Nkurunzinza, huku akisema kuwa muhula huo wa tatu unakiuka sheria na katiba ya taifa hilo.

Aidha, inaelezwa kuwa Rufikiri baada ya kutangaza uamuzi wake huo wa kumpinga rais Nkurunzinza naye alikimbia kusikojulikana.

Hata hivyo,  serikali ya nchi hiyo imeakanusha kuwa makamu wake hajatoroka nchini na kusema kuwa amesafiri nje kwa ziara rasmi ya kikazi.

Kumekuwa na mchanganyiko wa taarifa hizo kwani yeye Rufikiri amesema kuwa amekimbilia usalama wake akidai kuwa maisha yake yamo hatarini.

Taarifa hii imekuja baada ya serikali ya Burundi kususia mazungumzo ya amani kati yake na wapinzani yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname