HIVI NDIVYO WASANII NA WANAMICHEZO WATAKAVYONUFAIKA IKIWA LOWASSA ATAFANIKIWA KUWA RAIS

Tayari UKAWA jana Agosti 29, 2015 walifanya uzinduzi wa kampeni zao jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Jangwani, uzinduzi ambao ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi katika viwanja hivyo.

Mgombea urais kupitia umoja huo (UKAWA) alipata kuzungumza macheche katika uzinduzi wa kampeni hizo, lakini leo nimepita kwenye blog ya CHADEMA na kukutana na taarifa ambayo imeanika mipango yote ambayo Mhe Lowassa ataifanya endapo atafanikiwa kuwa rais.

Kwa sasa nimeamua kukusogezea hii mipango yake katika sanaa, utamaduni na michezo, soma hapa chini mwenyewe>>>

Tutaendeleza na kuwezesha vipaji vya sanaa na michezo.

Tutarudisha viwanja vya michezo vilivyovamiwa.

Tutafuta kodi zote za vifaa vya michezo.

Tutadhibiti viwango na maadili ya bidhaa za nje zinazoingizwa nchini na kuzitoza kodi halisia.

Tutajenga taasisi na vyuo vya kukuza michezo ili kuhakikisha kuwa ndani ya miaka mitano Tanzania. inashiriki kwa ushindi katika mashindano ya kimataifa ya soka na riadha.

Tutalinda hakimiliki za sanaa nchini.

Tutafuta kodi za sanaa kwa wasanii chipukizi ili kuwapa muda kwa kujijenga.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname