MTOTO WA MIAKA 9 KABAKWA NA KUAMBUKIZWA UKIMWI, MAHAKAMA IMEAMUA MAAMUZI HAYA ILI KUKOMESHA TABIA HIYO


Mahakama moja nchini Kenya imemhukumu mwanaume mmoja kifungo cha miaka 130 jela kwa kosa la kumbaka na kumuambukiza mtoto mwenye umri wa miaka 9 UKIMWI.

Mahakama hiyo kuu ya Kenya mjini Kisumu imemkuta na hatia bwana John Okewo mwenye umri wa miaka 25 na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 9 ambaye jina lake limehifadhiwa

Hakimu mwandamizi Aswani Opande alimkuta na hatia bwana Okewo kwa kumbaka mtoto huyo na akamhukumu kifungo cha miaka 100 jela. Katika shtaka la pili hakimu huyo mkuu wa eneo la Tamu lililoko Muhoroni alimhukumu mstakiwa kifungo cha miaka mingine 30 kwa kumuambukiza msichana huyo mwenye umri wa miaka 9 ugonjwa wa Ukimwi.

Hakimu alimpata na hatia bwana Okewo kutokana na kukiri makosa yake mwenyewe.

Aidha, upande wa mashtaka nao unasema kuwa bwana Okewo alimpa mtoto huyo pipi na biskuti mnamo tarehe 27 mwezi Machi kabla ya kumdanganya hadi akaingia chumbani mwake.

Naye mtoto aliyetendewa tukio hilo anasema alimtambua mshtakiwa kuwa mtu aliyemnunulia pipi na ''kumlalia''

Kwa sasa mtoto huyo anaendelea na matibabu maalum ya wanawake baada ya kujeruhiwa katika tukio hilo.

Sambamba na hayo, mshitakiwa alipopewa fursa ya kujitetee, mshtakiwa aliomba asamehewe kwani ni ''shetani aliyemdanganya'' kutenda maovu hayo. Hata hivyo Hakimu akakataa kabisa kumuonea huruma na akamhukumu kifungo cha miaka 130 jela ili iwe funzo kwake na kwa wengine wenye mawazo potofu kama yake.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname