Safari za yale mabasi yaendayo kasi zinatarajiwa kuanza leo Jumatatu ya Agosti 17 mabasi hayo yataanza kazi kuanzia saa 3
asubuhi nje ya kituo cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo.
Safari za mabasi hayo zitazinduliwa rasmi kwa kuanza kutoa huduma ya mpito na
baadaye wananchi wataruhusiwa kupanda mabasi hayo kutoka Ubungo kwenda
Kimara na kutoka Kimara hadi Kivukoni bila malipo.
Deusi Dedith Mutasingwa ambaye ni Afisa wa masuala ya fidia katika mradi
wa mabasi haya yaendayo haraka yaliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu
Tawala za Mikoa na serikali za mitaa,amesema yapo mabasi ya aina mbili
kuna yale ya mita 18 ambayo yana uwezo wa kubeba abiria 140 na yapo
yenye uwezo wa kubeba watu 80.
Aidha, amesema mabasi hayo pia yamezingatia watu wenye mahitaji maalum kama walemavu na wajawazito.
Mbali na hayo, kufuatia uzinduzi huo wafanyabiashara wanaopanga vitu vyao
pembeni ya barabara na kwenye vituo wameombwa kuviondoa na kwa wale
watakaonekana kukaidi amri hiyo faini yake si chini 250,000.
No comments:
Post a Comment