Ikiwa ni siku chache tu tangu msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz ambaye hivi karibuni ameachia nyimbo ya UTANIPENDA kuanza kutumia jina la “simba” kama ishara ya mtawala wa muziki wa bongo fleva kwakuwa amekuwa akifanya vizuri ndani ya tasnia hiyo na kumfanya aendelee kuwika kila siku katika game.
Ishu ya Diamond Platnumz kuanza kulitumia jina hilo imemfanya msanii nguli wa bongo fleva Mr Blue kuandika kupitia ukurasa wake wa instagram kuwa yeye ndiye aliyeanza kulitumia jina hilo mapema sana na hivyo kutumika kwa jina hilo kunamfanya ajinasibu kuwa ndiye mbunifu wa jina hilo na wengine wana muiga licha ya kwamba hakuweka bayana kuwa ni nani anayemuiga katika posti hiyo lakini kwa mujibu wa 'comment' zinazo endelea kuhusu hiyo post instagram zinaashiria kuwa ujumbe huo ulielekezwa kwa Diamond Platnumz
No comments:
Post a Comment