Habari za leo mpenzi msomaji wa habarimkusanyiko blog kama ilivyo kawaida lengo la blog hii ni kukuletea taarifa mbalimbali na hapa leo nimeona nikukusanyie hizi taarifa kuhusu mahusiano hususani zile kauli mbaya ambazo hazifai ndani ya mahusiano.
Tukiachana mimi na wewe lazima utajuta tuu!
Kauli hii maana yake nini? Maana hadi mtu anafikia kutoa kauli hiyo basi jua kuna jambo na kwa kifupi kauli hii humaanisha kwamba mtu huyo au mtoaji wa kauli hii kwamba anatamani kutoka kwenye mahusiano hayo lakini anashindwa au anakosa sehemu ya kaunzia ili kutoka na mtu wa namna hii mara anapopata tu nafasi basi lazima atatoka.
Kwa mtu unayempenda kwa dhati huwezi kumwambia ipo siku atajutia penzi lako kwani neno hili halistahili hata kidogo kwa wapendanao na ukiona unaambiwa hivyo jua siku zako zinahesabika.
Kauli nyingine ni ‘wee mwanamke una mdomo mdomo sana’
Kauli hii amra nyingi hutolewa zaidi na wanaume, jambo ambalo huashiria mwanaume kukerwa sana na maneno mengi ya mwenzi wake na ikiwa wewe mwanamke umeona umeanza kutamkiwa kauli hii na mwanaume wako basi jua hapo mapenzi tena hakuna.
Hata hivyo, ni vyema ifahamike kuwa wanaume wote huwa hawahitaji kuwa na mahusiano na wanawake wenye maneno mengi sana.
Tutakapo achana tambua sisi si wa kwanza kuachana
Kauli kama hii mwanaume hawezi kukuambia mkiwa kwenye mapenzi kwa mara ya kwanza, mara nyingi kauli hii huashiria kuchokana kwenye mahusiano.
Hivyo ikiwa unasikia kauli hii mara kwa mara katika mahusiano yako basi tambua kuwa penzi lako lipo kwenye hatari kuvunjika wakati wowote.
Kwani nilikukuta mtoto, tumejuana ukubwani
Wanaume wengi wanapenda kutumia kauli hii pale wanapowachoka wapenzi wao hasa wanapokuwa kwenye malumbano, bila shaka msomaji utakuwa na ushahidi wa hili hasa kwa wale waliowahi kukutana na maneno haya wataniunga mkono.
Ni maneno yanayouma na kujirudia kwenye ubongo wa mwanamke pia hupunguza mapenzi kwani mwanamke akitamkiwa hivyo mara kwa mara hujikuta ubongo unaanza kukubali na kupunguza mapenzi kwa yule aliyekuwa akimpenda.
Sasa ili kuepukana na hayo yote na kusababisha mahusiano kuvunjika mara kwa mara ni vyema kuhakikisha unaepuka kauli mbaya kwa Yule unayempenda kwani maneno mabaya ni sumu ya mapenzi na ikiwa utatamka kwa bahati mbaya labda kwa sababu ya hasira ni vyema kuomba msamaha wa dhati kabisa kwa mwenzi wako ili kutoharibu mahusiano yako.
No comments:
Post a Comment