Jana Desemba 29 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa msanii na mbunge wa Mikumi,Mh Joseph Haule maarufu kama Professor Jay ambaye aliamua kutumia siku hiyo kwa kufanya maamuzi ya kufanya usafi kwenye ofisi yake aliyokabidhiwa huko jimboni kwake Mikumi Morogoro.
Kupitia ukurasa wake wa instagram mbunge huyo aliandika maneno haya "Asante sana Mungu leo nimetimiza miaka 40 tangu nimezaliwa …. I dedicate this birthday kwa watu wangu wote wa MIKUMI na leo ndio tumeifungua rasmi ofisi ya MBUNGE wa MIKUMI baada ya kukabidhiwa Funguo na kuifanyia Usafi kwa pamoja tayari kwa kusikiliza changamoto za wana mikumi, Ushauri na maoni ya jinsi gani tunashirikiana pamoja na wana Mikumi kuweza kuleta mabadiliko na maendeleo ya MIKUMI YETU… EEE MWENYEZI MUNGU TUSAIDIE" @professorjaytz
No comments:
Post a Comment