ENOCK BELLA WA YAMOTO BAND HAWEZI KUSAHAU HIKI NDANI YA MWAKA 2015

Mwaka 2015 ndio unaisha leo na safari inaelekea ndani ya mwaka mpya 2016 , lakini kwa kawaida mwaka unapoisha kila mtu huwa anakuwa na mambo yake ambayo hawezi kuyasahau ambayo yametokea ndani ya mwaka mzima.

Kwa upande wa Enock Bella wa yamoto Band naye anacho kitu ambacho hawezi kukisahau ambacho kimetokea ndani ya mwaka huu 2015.

Eneck Bella anasema kuwa "Siwezi kusahau mwaka huu nimempoteza marehemu mama yangu iko ndio kitu sitokuja kukisahau milele daima mpaka naingia kaburini kwa sababu yeye ndio mwanamke wangu wa nguvu….wakati yupo mama tulikuwa tunaishi vizuri maisha safi kwa raha pindi mama alivyotoweka tu familia imeparaganyika mimi naishi kwangu namdogo wangu wadogo zangu wengine wanaishi kivyao, father wangu anaishi kivyake na bro wangu yaani ndio sitokuja kusahau katika maisha yangu"

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname