KAMANDA KOVA ASTAAFU KAZI JESHI LA POLISI, MANENO YAKE MWENYEWE YAPO HAPA

Leo ni siku ya mwisho kwa Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam Kamishina Suleiman Kova, kulitumika Jeshi la Polisi nchini kutokana na muda wake wa kulitumikia taifa kupitia jeshi hilo kufikia kikomo.

Kamanda Kova ametoa taarifa hiyo leo asubuhi alipokuwa akizungumza asubuhi kupitia  kipindi cha  kumekucha cha ITV, na kusema kuwa mkataba wake na Jeshi la Polisi umeishia leo, hivyo analazimika kukaa pembeni.

"Mmepata bahati sana, maana wakati nakuja Dar es salaam mwaka 2008 nikitokea Mbeya, kwa mara ya kwanza nilifanya kipindi hapa na leo hii nawaagia hapa, leo ndio siku ya mwisho kwangu kulitumikia jeshi la Polisi, mkataba wangu na jeshi la Polisi unaisha leo, lakini siwaachi hivi hivi, Kaimu wangu yupo atakuwa nanyi",
alisema Kamanda Kova.

Kamanda Kova amekuwa  Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam, na kwa kipindi chake chote akitumikia jeshi hilo amefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya uhalifu, yaliyokuwa yanaitikisa nchi hususani matukio ya wizi na uvamizi wa taasisi za fedha benki.

CHANZO: www.eatv.tv

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname