Showing posts with label ukatili. Show all posts
Showing posts with label ukatili. Show all posts

WANAWAKE WALIOKEKETWA SASA KUTOOLEWA



Spika wa Bunge la Uganda Bi Rebecca Kadaga amewashauri wanaume kutowaoa wanawake waliokeketwa akiwataja kuwa ni mzigo ambao hauwezi kuijenga jamii. 

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, Spika Kadaga alitoa wito huo wakati wa sherehe za kitamaduni ambazo huandaliwa na mfuko wa umoja wa mataifa unaosimamia idadi ya watu na wahisani wengine, huku lengo likiwa ni kupinga ukeketaji .

''Mwanamke ambaye amekeketwa hana thamani yoyote. Achaneni na wanawake waliokwenda kukeketwa na badala yake chagueni wanawake ambao hawakukeketwa na ambao wanaweza kuimarisha jamii'', alisema Bi Kadaga.

Nchini Uganda, utamaduni wa ukeketaji hufanyika mashariki mwa nchi hiyo na katika makabila matatu ikiwemo lile la Pokot, Sabiny na Tepeth hususani katika wilaya za Kampchorwa, Kween na Bukwo.

Utamaduni huo unaojulikana kama upashaji tohara wanawake umekithiri miongoni mwa tamaduni nyingi na bara la Afrika kwa ujumla na hutumika kumuandaa mwanamke anayeolewa ama hata kuonesha kwamba, mwanamke amekua.

Mbali na hayo, Bi Kadaga ambaye aliandamana na Waziri wa Maswala ya Kijinsia, Rukia Nakadama wote walitia sahihi ya kumaliza ukeketaji nchini Uganda, huku wakiwaonya wazazi katika eneo hilo kukoma kuwalazimisha watoto kuingia katika ndoa za mapema na badala yake kuwataka kuwapeleka shule.

Sambamba na hayo, baadhi ya wanawake waliokuwa wakitekeleza tendo hilo waliiomba serikali kulisaidia kundi la watu ambao wameacha kuwapasha tohara wanawake.

Asante kwa kuendelea kutembelea blog hii, tunakuhakikishia kuendelea kukupatia habari zaidi.

MTOTO AUWAWA KIKATILI NA MWILI WAKE KUTELEKEZWA





Arusha, Na Theo .M.George.

Mtoto mwenye jinsia ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja amekutwa amekatwa sehemu za kifuani na kubaki kiwiliwili na miguu tu, na mtu asiyejulikana.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani, Arusha Liberatusi Sabasi, alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo Novemba 30 mwaka huu majira ya saa 6:30 mchana katika maeneo ya Kimindolosi Olasiti katika halmashauri ya jiji la Arausha, ambapo mtoto mchanga huyo alikutwa ametupwa shambani huku akiwa amefariki dunia.

Kamanda Sabasi alisema kuwa, mwili wa mtoto huyo uligundulika baada ya watoto wadogo ambao walikuwa wanachunga mbuzi katika eneo hilo na kuoona mwili huo na kisha kutoa taarifa kwa balozi wa nyumba kumi wa mtaa huo aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Hamis Mhilo,

Taarifa zinaasema kuwa balozi huyo baada ya kupata taarifa hiyo aliamua kutoa taarifa katika kituo cha jeshi la Polisi.

Hata hivyo, baada ya askari kufika eneo la tukio walikuta mwili wa kichanga hicho kikiwa kimekatwa sehemu za kifuani na kubaki kiwiliwili na miguu tu.

Sambamba na hayo, Jeshi la Polisi mkoani Arusha limesema kuwa linaendelea na upelelezi ili kuweza kubaini chanzo cha tukio hilo pamoja na watu waliohusika katika tukio hilo,.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi.

Ni wajibu wetu kuhakikisha unapata habari zote katika kila kona ya Tanzania, tafadhali endelea kuungana na habarimkusanyiko.blogspot.com kwa habari nyingi zaidi.

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname