Afya ya Kikwete sasa safi
Akitoa hotuba yake kwa Taifa akiwa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ambapo pia hotuba hiyo ilitangazwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa TBC, Kikwete amesema aligundua kuwa na hatua ya pili ya saratani ya kibofu ambayo baadaye ikaonekana kuwa ni hatua ya kwanza.
Aidha, Kikwete aliongeza kuwa madaktari wamesema “saratani haikuenea katika sehemu nyingine za mwili na baada ya upasuaji sasa wamesema nimepona saratani”
Hata hivyo, ameongeza kuwa aligundulika kuwa na saratani ya kibofu zaidi ya mwaka mmoja uliopita na alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins Hospital tarehe 8 Novemba.
Rais Kikwete mwenye umri wa miaka 64, pia amewataka wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao ili wagundue maradhi mapema.
Habarimkusanyiko.blogspot.com ipo pamoja nawe katika kupashana habari katika nyanja zote, kijamii, kisiasa na kiuchumi tafadhari sana ungana nasi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment