Je, ulipitwa na hii harusi iliyofanyika katika bwawa lenye lita milioni 1.5 za maji ya bahari ?



Katika hali ya kushangaza harusi  hiyo ya Bi Dorota Bankowska ambaye ni mpiga mbizi mzoefu aliolewa na mpenzi wake ambaye ni mwalimu James Abbot nyumbani kwao mjini Plock , Poland mwezi  jana, huku wakieleza kuwa lengo kuu la kufanya hivyo ni kusheherekea harusi yao hiyo
 


Taarifa zinasema kuwa bwawa lililotumika kufanyia harusi hiyo, hutumiwa katika kutoa mafunzo kwa wapiga mbizi pamoja na kufanyia majaribio ya vifaa vipya.

Kuhusu katika mavazi inaelezwa kuwa maharusi hao walipendeza baada ya Bi harusi kuvaa gauni nyeupe, huku bwana harusi naye akivalia sketi ambayo huvaliwa na waskochi ijulikanayo kama 'Kilt'



Pia harusi hiyo iliwahusisha marafiki ambao ni Ala Bankowska na Charlie Cran-Crombien huku wote wakisheherekea chini ya maji hayo wakiwa wamevaliaa vifaa maalum vya kupiga mbizi pamoja na mavazi ya harusi.



Harusi hiyo inaelezwa kutazamwa na takriban wageni 100 wakiwa nje ya maji.

Hii ndio maana ya mkusanyiko wa habari, tafadhari endelea kuungana nasi uzidi kupata habari mbalimbali kutoka hapa nchini Tanzania na hata nje ya mipaka ya nchi yetu

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname