Taswira kuhusu sakata la Escrow

Siku tatu zilizopita kila Mtanzania katika mitaa na mikoa mbalimbali hapa nchini ailikuwa katika harakati za kutaka kujua kilichokuwa kikiendelea kutokea Bungeni mjini Dodoma wakati wabunge walipokuwa wakijadili kuhusu sakata la matumizi mabaya ya fedha za umma zilizochukuliwa kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow zinazofikia kiasi cha Sh306 bilioni.

Hali ilikuwa kama hivi.....

Kuna wale ambao walikuwa wakikusanyika katika eneo moja na kufuatilia kwa umakini matangazo hayo.


Pia kuna wale ambao walitaka kuhakikisha hata zile redio zao mbovu zinawaka ili kufuatilia mjadala huo


 Na wale ambao walikuwa katika mihangaiko yao ya kila siku ya kutafuta mkate wa siku, nao hawakutaka kupitwa, kwani walikuwa na vifaa vya kusikilizia redio masikioni (earphone) kupitia simu zao muda wote.




Hivyo ndivyo hali ilivyokuwa kwa baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini pindi walipokuwa wakifuatilia sakata hilo.

Tafadhari endelea kuungana nasi katika kupashana habari mbalimbali, na tutafurahi endapo utamjuza na mtu wako wa karibu kuhusiana na habarimkusanyiko.blospot.com

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname