Upendo Nkone kushiriki uzinduzi wa albamu ya “Nifuraha na Shangwe”



Tanga

Muimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini Tanga Mwalimu Magreth Peter Singano, amesema anataraji kusindikizwa na muimbaji mwenzake wa nyimbo za injili nchini Upendo Nkone katika kuzindua albamu yake ya tatu ambayo itakuwa ni zawadi ya sikuku ya Krismasi kwa wapenzi na wadau wa muziki huo wa nchini
Mwl, Magreth Peter Singano anayetaraji kuzindua albamu yake ya "Nifuraha na Shangwe"

Akizungumza Jumapili hii, muimbaji huyo amesema kuwa, albamu hiyo itazinduliwa rasmi Desemba 7 mwaka huu (2014) na itafahamika kwa jina la “NIFURAHA NA SHANGWE” , huku ndani yake ikihusisha nyimbo 8 zenye kumsifu na kumtukuza Mungu.

Aidha, akifafanua zaidi kuhusu uzinduzi wa albamu hiyo Mwl, Magreth Peter Singano amesema, kuwa shughuli zote za uzinduzi zitafanyika katika ukumbi wa Naivera Complex uliopo mtaa wa Bomba mjini humo na wataanza majira ya saa 7: 30 mchana na kuendelea, huku kiingilio kikiwa ni shilingi 3,000 kwa watu wazima na watoto shilingi 1,000.

Mbali na hayo, Mwl, Magreth Peter Singano amewataja wasanii wa injili watakaomsindikiza katika uzinduzi wa albamu hiyo kuwa ni pamoja na mwimbaji Upendo Nkone, kutoka jijini Dar es Salaam na kwaya mbalimbali kutoka ndani ya jiji hilo wa Tanga.

Upendo Nkone, ambaye atamsifu Mungu siku hiyo ya uzinduzi wa albamu ya "Nifuraha na Shangwe"

Akielezea historia yake fupi tangu alipoanza kujihusisha na kumtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji, Mwl, Magreth Peter Singano anasema “mnamo mwaka 1990 nilijiunga na kwaya ya Mtakatifu Agustino ya kanisa la Aglikana lililopo Chumbageni mkoani Tanga”



Hata hivyo, Mwl, Magreth Peter Singano anaendelea kusema kuwa, ilipofika mwaka 2006 ndipo alipoanza rasmi kuimba yeye mwenyewe, huku akiongeza kuwa hamasa ya kuanza kuimba kama muimbaji wa kujitegemea aliipata mara baada ya kusikiliza wimbo wa mwimbaji wa muziki wa injili Angela Chibalonza uitwao “YAWE UHIMIDIWE”



Albamu hiyo inayokwenda kuzinduliwa Desemba 7 itakuwa ni ya tatu kwa muimbaji huyo, ambapo hapo kabla alifanikiwa kutoa albumu yake ya kwanza iliyoenda kwa jina la “KIMBILIO LANGU” na kufuatiwa na nyingine ambayo ilitoka mwaka 2013 iliyokwenda kwa jina la “SONGA MBELE” ambazo zote zilionekana kufanya vizuri katika soko la muziki wa injili hususani jijini Tanga na baadhi ya mikoa mingine hapa nchini.

Source: philimaro.blogspot.com

Lengo la habarimkusanyiko.blogspot.com ni kuhakikisha unapata habari za kila kona hapa nchini, tafadhari endelea kufuatana nasi kwa mengine mengi  mazuri kadri siku zinavyozidi kuja, lakini pia ni vizuri ukamjuza na mwenzako kuhusu blog hii ili naye asipitwa na habari mbalimbali asante kwa kutuunga mkono.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname