Msichana wa kazi za ndani aliyemtesa mtoto, sasa aanika wazi sababu za yeye kufanya kitendo hicho.



Baada ya vyombo vya habari mbalimbali duniani kuripoti kuhusu lile tukio la msichana wa kazi za ndani, kumtesa mtoto nchini Uganda, hatimaye msichana huyo naye ameweka bayana sababu zilizompelekea kumtesa mtoto Arnella Kamanzu.

Msichana huyo Jolly Tumuhiirwe, ambaye kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi, amesema sababu iliyomfanya amtese mtoto Arnella Kamanzi, ni kutokana na kuchanganyikiwa baada ya waajiri wake kutompatia pesa ili amtumie baba yake ambaye alikuwa anaumwa.

Hata hivyo, Jolly amesema anajihisi mwenye hatia kwa kile alichokifanya japo anadhani alifanya hivyo kama njia ya kumkanya mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimuona mama wa mtoto huyo akimpiga kama njia ya kumkanya.

Aidha, mbali na hayo, Jolly amesema amekuwa akijisikia vibaya pale ambapo wafungwa wenzake wamekuwa wakimtenga na kutaka kumpiga.

Endelea kuungana na habarimkusanyiko.blogspot.com, kwa habari nyingine nyingi kila wakati, pia itakuwa ni njema na haki endapo utamjulisha na ndugu jamaa au rafiki kuhusu blog hii, asante kwa kuwa nasi.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname