Wanaume wahusishwa na usambazaji wa Ebola
Imeelezwa kuwa, idadi kubwa ya wanawake wameonekana kuendelea kuambukizwa virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola na waume zao, ambao ni manusura wa ugonjwa huo nchini Liberia.
Kwa mujibu wa Dkt. Anne Atai Omoruto, mtaalam wa afya kutoka nchini Uganda ambaye kwa sasa yupo kwenye kituo cha matibabu cha Island Clinic mjini Monrovia, Liberia, amesema kwamba wamekuwa wakiona idadi kubwa ya wake za wanaume walionusurika na ugonjwa wa Ebola wakifika kwenye kituo hicho wakiwa wameambukizwa virusi vya ugonjwa huo.
Dk, Omoruto akifafanua zaidi juu ya maambukizi hayo alisema kwamba, sababu ya hali hiyo ni kutokana na tabia ya baadhi ya wanaume manusura wa ugonjwa wa Ebola kutotumia mipira ya kondomu pale wanapojamiana na wake zao.
Aidha, daktari huyo aliendelea kueleza kuwa wamaekuwa wakiwashauri wanaume waliopona kutokana na kirusi cha Ebola kujiepusha na vitendo vya ngono au kutumia kinga ya mipira ya kondomu pindi wanapohitaji kujamianaa, lakini hali imekuwa tofauti kwani wanaume wengi wameshindwa kufuata maagizo hayo, hivyo kusababisha wake zao kuendelea kuwasili kwenye kituo cha matibabu.
Mbali na hayo, pia Shirika la Afya Duniani (WHO) hivi karibuni lilitangaza kuwepo kwa idadi ya watu inayokaribia 7,000 waliopoteza maisha yao kutokana na homa hatari ya Ebola huko magharibi mwa Afrika.
Jukumu letu ni kuhakikisha unapata habari muda wote ndani ya siku saba za wiki, tafadhari endelea kuungana na habarimkusanyiko.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment