Watu wengi kwa sasa wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la msongo wa mawazo ‘stress’ jambo ambalo limesababisha madhara makubwa katika maisha yao na baadhi ya watu kufikia hatua ya kupoteza maisha.
Tatizo hili la msongo wa mawazo ‘stress’ linaelezwa kuwa ni tatizo kubwa na mbaya zaidi watu walio wengi hulichukulia kirahisi rahisi, lakini kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wanasema kuwa, huenda itakapofika mwaka 2020 basi tatizo hili litakuwa linashika nafasi ya pili kwa kusababisha vifo kwa watu hususani katika nchi zinazoendelea.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa tatizo hili huchangia sana kushuka kwa uwezo wa mtu hasa kuwajibika katika majukumu mbalimbali yakiwemo ya kimaisha, huku ikibainishwa kuwa tatizo hili pia limekuwa likichangia zaidi moja ya kumi katika kuvuruga muda wa uzalishaji duniani.
Aidha, taarifa za uhakika zinasema kuwa zaidi ya nusu ya watu wenye tatizo hili huwa hawajui kwamba wanalo na hata wale walio karibu yao kiuhusiano huwawia vigumu pia kujua kwamba, wenzao wako kwenye matatizo. Sasa hapo ndipo swali linapokuja je, wewe upo kwenye usalama kiasi gani ? na endapo ukifahamu kwamba unatatizo hili ni vipi utaweza kujiokoa?
Habarimkusanyiko.blogspot.com leo hii imeona ni vyema kukupatia baadhi ya dalili ambazo ukiziona ujue basi moja kwa moja umeshapata tatizo hili la msongo wa mawazo ambazo ni hizi hapa zifuatazo:
1. Kukosa nguvu na kujihisi huna uwezo wa kufanya shughuli yoyote au mambo mengine.
2. Kujihisi mwenye huzuni kwa kipindi cha muda mrefu
3. Kupoteza matumaini na kujiona huna thamani
4. Kushindwa kufurahia baadhi ya vitu, ambavyo hapo awali ulikuwa ukivifurahia
5. Kushindwa kuzingatia mambo, mfano masomo kwa wanafunzi, mazungumzo au shughuli yoyote.
6. Kukosa uwezo wa kufanya maamuzi hata kwa yale mambo madogo
7. Kujihisi unakosa amani na kujikuta ukikereka tu kwa muda wote
8. Kulala kupita kiasi, ingawaje hii si sana kwani wengi wenye tatizo hili mara nyingi hupoteza usingizi kabisa
9. Maumivu ya baadhi ya maeneo ya mwili ambayo hayana sababu wala chanzo cha moja kwa moja
10. Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa kiwango kikubwa
11. Kupoteza hamu ya kula jambo ambalo huweza kusababisha udhaifu wa mwili kwa mhusika
12. Kuwa na mawazo ya kutaka kujiuwa
Kimsingi hizo ni baadhi ya dalili za mtu mwenye msongo wa mawazo ‘stress’ nadhani utakuwa umejitathimini na kujitambua endapo na wewe kama upo kwenye ‘list’ ya watu wenye tatizo hilo au laa! Lakini kama umebaini kuwa unatatizo hilo usipate shida kwani habarimkusanyiko.blogspot.com imekuandalia namna ya kukabiliana na ‘stress’ kama ifuatavyo:
Tafiti mbalimbali za kifasihi zinaonesha kuwa, njia ya ushauri ni bora zaidi, kuliko njia nyingine yoyote
Baadhi ya njia zinazopendekezwa katika kutatua tatizo hili ni kama zifuatazo;
1. Pendelea kufikiri vizuri, jaribu kusoma na kusikiliza kazi mbalimbali zenye kutia moyo na kukufanya kuamini zaidi kwamba binadamu tunaweza, hakikisha unaepuka kutazama, kusikiliza kazi ambazo zinaonesha upande mmbaya tu wa kimaisha.
2. Ushughulishe mwili wako zaidi, kuna ushahidi wa kitaalam ambao unaonesha kwamba, shughuli za kimwili zinaweza kuwa msaada mkubwa wa kupambana na msongo wa mawazo. Kwa mujibu wa ripoti ya “Achives of Internal Medicine” ya mwaka 1999 inaainisha kuwa, mazoezi ya mwili yanapunguza au kufuta dalili za msongo wa mawazo kwa wastani sawa kabisa na ule wa matumizi ya vidonge vinavyopendekezwa kwa tatizo hilo. Hivyo endapo upo kwenye msongo wa mawazo unaweza kufanya mazoezi ya kutembea angalau nusu saa , mara tatu kwa wiki, pamoja na mazoezi ya viungo japo kwa dakika 15 kila siku, endapo utafanya hivyo kwa wiki 5 mfululizo lazima utaona mabadiliko.
Angalizo:
Kabla hujaamua kuanza mazoezi yoyote ni vizuri kupata ushauri kwa wataalam wa afya, lakini unaweza kuanza mazoezi ya kutembea kila siku kabla ya kuwaona wataalam hao, tembea kilometa 6 au zaidi kila siku asubuhi tu au ukipendelea asubuhi na jioni.
3. Njia nyingine ya kupunguza msongo wa mawazo ni pamoja na kuanza kujilazimisha kufanya yale ambayo unayafurahia au yanayokuvutia katika maisha.
Kwa makala zaidi za kuelimisha endelea kuungana nasi, na ni vizuri ukamjulisha mtu wako wa karibu kuhusu blog hii

No comments:
Post a Comment