ASILIMIA 97 YA WAHITIMU WA DARASA LA SABA WAFANIKIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2015



Jumla ya wanafunzi 438,960 kati ya wanafunzi 451,392 waliohitimu elimu ya msingi mwaka huu wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwakani, huku idadi hiyo ikielezwa kuwa ni sawa na asilimia 97 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani huo.

Taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa waandishi wa habari imesema kwamba ufaulu huo umeongezeka kwa asilimia 1.08 ikilinganishwa na mwaka jana.

Licha ya kuongezeka kwa ufaulu huo, imeelezwa kwamba jumla ya wanafunzi 12, 432 waliofaulu, hawajapata nafasi ya kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo upungufu wa majengo, hali inayowalazimisha kusubiri chaguo la pili litakalofanyika mapema mwakani.

Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa jumla ya wanafunzi 808,085 walisajiliwa kufanya mtihani wa Taifa mwaka 2014, lakini ni wanafunzi 792,122 tu ndio waliofanya mtihani, hiyo ikiwa ni asilimia 98.02% ya wanafunzi wote waliosajiliwa.

Pamoja na hayo taarifa ya Tamisemi ilibainisha kuwa wavulana wanaongoza kwa kuchaguliwa zaidi ya wasichana, ambapo jumla ya wavulana 219,964 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 97.28 ya wanafunzi wote waliochaguliwa huku wasichana wakifikia 218,996 ambayo ni sawa na asilimia 97.1 ya wanafunzi waliochaguliwa.

Asante kwa kuendelea kutembelea habarimkusanyiko.blogspot.com, tunaomba uendelee kutuunga mkono



No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname