PROF: TIBAIJUKA ATOA MSIMAMO WAKE KUHUSU SAKATA LA ESCROW


Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
Baada ya Mwanasheria Mkuu Jaji Fredrick Werema kujiuzuri, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa mara nyingine amejitokeza hadharani na kutoa msimamo wake kwamba hana sababu ya kujiuzuru kwenye nafasi yake kwa kuwa hakuhusika kwa namna yeyote kwenye sakata la uchotwaji wa mabilioni kwenye akaunti ya Escrow.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Profesa Tibaijuka, amesema pamoja na kuwepo kwa shinikizo la kutaka kujiuzuru, yeye binafsi ameona hana sababu ya kufanya hivyo kwani kwa kufanya hivyo sawa na kukubali kuwa amehusika moja kwa moja kwenye kashfa hiyo jambo ambalo si la kweli.

Aidha, Profesa Tibaijuka amesema kuwa uvumi unaoendelea kusambazwa mitaani ni ishara mbaya kwani unawaaminisha wananchi kuwa amehusika katika sakata hilo wakati yeye hajahusika na jambo lolote.

“Huu uvumi unatakiwa kuachwa, sioni sababu yeyote ya mimi kujiuzuru kwa kuwa sijahusika kwa namna yoyote kwenye sakata hili la Escrow” alisema Profesa Anna Tibaijuka.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname