ASKOFU AISHI NA TATIZO LA TEZI DUME NDANI YA MIAKA 15




Askofu Mkuu Mstaafu wa Cape Town, Desmond Tutu, amelazimika kuahirisha mipango ya ziara zake kwa mwaka mzima ujao kutokana na sababu za kiafya.
Taarifa iliyotolewa na taasisi yake imeeleza kuwa Askofu huyo anakabiliwa na tatizo la tezi dume ambayo ameshadumu nayo miaka kumi na mitano iliyopita, na hivyo ataanza matibabu hivi karibuni ili kukabiliana na tatizo hilo.
Askofu Desmond Tutu
Mbali na hayo habari ziliendelea kusema kuwa, binti wa Askofu huyo amemuelezea baba yake mwenye umri wa miaka themanini na miwili, kwamba hatahudhuria tuzo za Nobel zitakazo fanyika baadaye wiki hii huko Rome, Italia.

Ni vizuri ukamshirikisha ndugu, jamaa, na hata rafiki pia kuhusu uwepo wa blog hii ya habarimkusanyiko.blogspot.com, tambua ya kuwa tunathamini sana mchango wako wewe msomaji wetu na tunakusihi endelea kuwa nasi siku zote 

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname