MWANAMKE ATELEKEZWA BWAWANI KWA KOSA LA KUSHINDWA KUJIFUNGUA MTOTO WA KIUME



Polisi Mashariki mwa mji wa Calcutta nchini India, wanachunguza tukio la mwanamke ambaye jamii yake iliamua kumtelekeza katika bwawa, kwa madai ya kuwa mwanamke alishindwa kuzaa mtoto wa kike ambaye baadaye walitemtegemea kuwa kahaba.

Jamii ya familia ya mwanamke hiyo inaelezwa kuwa hutegemea watoto wao wa kike kwa kufanya kazi ya ukahaba.

Mwanamke huyo aliiambia BBC, kwamba familia ya wakwe zake walianza kumdhihaki baada ya kuzaa watoto wa kiume watatu mfululizo, na kufahamishwa kwamba familia hiyo kwa kawaida huwapeleka watoto wa kike wa ukoo wao kufanya kazi ya ukahaba, iweje yeye azae watoto wakiume watupu?

Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa mwanamke huyo aliokolewa na chama cha kujitolea kuwahudumia makahaba kabla hajalazimika kujitosa kwenye ukahaba kamili.


Je habari hii imekugusa kwa kiasi gani? Unaweza kutoa maoni yako na itakuwa ni nzuri zaidi nasi tukisikia chochote kutoka kwako msomaji wetu

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname