JB: AJIBU KILE ALICHOKISEMA ZAMARADI KUHUSIANA NA FILAMU ZA HAPA NCHINI KUTOFANYA VIZURI KIMATAIFA





Hivi karibuni mwanadada Zamaradi Mketema ambaye ni mdau wa filamu hapa nchini, alifunguka yake ya moyoni kuhusiana na tasnia ya filamu hapa nchini kutofanya vizuri hususani katika nyanja ya Kimataifa, hatimaye mwigizaji mkongwe nchini Jacob Steven maarufu kama JB ameamua kuandika haya yafuatayo kuhusiana na hicho alichokisema Zamaradi Mketema siku chache ziliozopita.

Msanii Jacob Steven JB

Zamaradi Mketema mtangazaji wa Take One Clouds Tv na mdau wa filamu nchini

Hiki ndicho alichoandika JB………..

“Kwako Zamaradi na wengine wote.

Kwanza napenda niwashukuru wote kwa jinsi mnavyotuwazia mema. Naomba nichukue nafasi hii kuwapongeza waigizaji wote wa Tz na waandaaji wa filamu kwa kuthubutu kutengeneza filamu hizi katika mazingira magumu. Najua watanzania wengi wangependa kuona tukipeperusha bendera nje,lakini naomba muwape wasanii muda.

Tasnia hii ni changa na ina changamoto ambazo zinakatisha tamaa. Hebu tujiulize kwa nini wasomi wengi waliosomea filamuu UDSM na BAGAMOYO hawafanyi filamu hizi? Wasambazaji wengi wakubwa mamu,wananchi na hata hans pop walijaribu wakakimbia, kuna producer mkubwa hapa nchini JOHN RIBER ambaye ametengeneza filamuu kama NERIA na YELLOW CARD lakini naye ukimwambia njoo kwenye hizi filamu atakupa jibu.

Nakubali tuna makosa mengi kama ubora wa filamu zetu na stori lakini nataka niwaambie mazingira ya kufanya filamu bongo yanakatisha tamaa wizi wa kazi zetu umezidi na wasambazaji wengi wamekimbia. Binafsi najipanga kuwa mtayarishaji zaidi kuliko mwigizaji kwa sasa kupitia JERUSALEM FILMS na ndio maana filamu nyingi natoa nafasi kwa vijana ambao kama mabadiliko ya sera ya filamu yatafanywa watatuwakilisha nje.

Kiswahili kisichukuliwe poa kwani kina nafasi kubwa sana. Tukumbuke SHARUK KHAN ni ‘actor’ tajiri2 duniani lakini filamu zake ni za kihindi. Hebu sote tusaidiane kupambana na changamoto hizi na tuanze na EAST AFRICA kwanza huku tukiboresha, wasomi wa filamu msikimbie njooni tuanze wote na tuwape moyo wasanii wetu waliojaribu kusimamisha tasnia hii kwa vimtaji toka mifukoni mwao na vipaji walivyopewa na Mungu bila msaada kutoka popote. Asanteni kwa kutuunga mkono kwemye filamu zetu.”

Alimaliza kwa kusema JB.

Hayo ndiyo aliyofunguka JB, kuhusiana na tasnia hiyo ya fiamu, Je unawazo gano kuhusiana na aliyoyasema JB juu ya suala hili ni vizuri ukatoa maoni yako pia

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname