TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUTOKA MKOANI MBEYA




MTU MMOJA MKAZI WA CHAPWA – TUNDUMA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA JULIUS LABISON HAONGA (34) AMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.317 CNS AINA YA MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA JOACHIM MKENYA KUACHA NJIA NA KISHA KUPINDUKA ENEO LA CHAPWA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.

AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 09.12.2014 MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO MAENEO YA CHAPWA – TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WATAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
TAARIFA ZA MISAKO:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU AMBAO NI 1. ATUPAKISYE KAJOLO (22) MKAZI WA KIJIJI CHA BUTULO-MBOYO 2. LWITIKO SIMON (25) MKAZI WA KIJIJI CHA IBILILO NA 3. ESSAU JOHN (32) MKAZI WA KYIMO WAKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO MOJA [1KGM] IKIWA KWENYE MFUKO WA RAMBO.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 09.12.2014 MAJIRA YA SAA 14:30 MCHANA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA ENEO LA KIWIRA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname