DR CHENI: "NIMEKUBALI KUOLEWA" SASA IMERUHUSIWA KUTOKA



Baada ya Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) kuzuia kutoka kwa filamu ya “Nimekubali Kuolewa” ya msanii Mahsein Awadh Said au maarufu kama Dr. Cheni , hatimaye bodi hiyo imemruhusu msanii huyo kuitoka filamu hiyo baada ya kukamirisha matakwa ya bodi hiyo.

“Nimefanikiwa kuipigania filamu yangu ya ‘Nimekubali Kuolewa’, itatoka mwezi wa pili mwakani. Kikubwa nilichokifanya ni kurekebisha baadhi ya vitu ambavyo walihitaji na imekamilika kwahiyo watu wakae mkao wa kula tu,” alisema Dr Cheni.
 


Nimuonekano wa "Nimekubali Kuolewa"
Mbali na hayo, Dr Cheni alisema kwamba, kuzuiliwa kwa filamu hiyo kulimnyima raha kiasi cha kumfanya asifanye kazi nyingine mpaka akamirishe kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname