MAAFISA WA POLISI WASHUTUMIWA KUFANYA MAUAJI NCHINI KENYA





Shirika la habari la Al Jazeera limeweka bayana ripoti yake ambayo imehusisha maafisa wa usalama wa Kenya na mauaji ya viongozi wa dini ya kiisilamu pamoja na washukiwa wa ugaidi.

Taarifa hiyo ya ufichuzi iliyopeperushwa Jumatatu, ilionesha baadhi ya maafisa wa polisi wanaofanya kazi yao kwa usiri mkubwa wakikiri kuwaua baadhi ya viongozi wa kiisilamu wanaosemekana kufunza mafunzo yenye itikadi kali ya kiisilamu pwani ya Kenya.

Ripoti hiyo http://goo.gl/wYV91g ambayo ilikuwa ni kanda ya video yenye polisi hao wakikiri kuwaua waisilamu mjini Mombasa, iliwekwa kwenye mtandao wa YouTube na shirika hilo na inaonesha sura za polisi hao zikiwa zimefichwa huku wakisimulia ambavyo wamekuwa wakiwaua watu wanaonekana kuwa wenye kutoa mafunzo ya itikadi kali na wanaotatiza usalama wa nchi.

Mmoja wa maafisa alisema wamewaua washukiwa wengi sana wa ugaidi akiwemo Sheikh Abubakar Shariff Makaburi mnamo mwezi April.

Taarifa hizo zilichapishwa kwenye vyombo vingine vya habari vikizungumzia mauaji ya kisiri ya washukiwa wa Ugaidi yanayofanywa na maafisa wa polisi waliopata mafunzo ya hali ya juu nchini Kenya.

Habari zinaarifu kuwa baadhi ya maafisa hawo wanatoka kitengo cha Polisi cha kupambana na ghasia au GSU na Shirika la Kitaifa la Ujasusi.

Aidha, inaelezwa kwamba mmoja wao alinukuliwa akisema katika kundi hilo .''sisi hupewa taarifa tu na kisha kutekeleza matakwa ya wakuu wetu. Huwa tunamuua yule mshukiwa tuliyetumwa kumuua na kazi hii huwa tunaifanya kwa usiri mkubwa sana,''

Pamoja na hayo, walihojiwa wote walikiri kupokea mafunzo ya hali ya juu mno kabla ya kufanya kazi yao kwa umakini mkubwa.

Sambamba na hayo, ripoti hiyo ya Al Jazeera inasema kuwa, washukiwa wa ugaidi huuawa badala ya kupelekwa mahakamani.

Sio mara ya kwanza kwa mashirika ya usalama nchini Kenya kutuhumiwa kwa mauaji ya washukiwa wa ugaidi kwa siri.Hata hivyo, Serikali ya Kenya imetoa taarifa kupinga ripoti hiyo inayodai kuwa polisi nchini humo walihusika na mauaji ya washukiwa wa ugaidi.

Ripoti hiyo pia iliyooneshwa na runinga ya al jazeera na ilidai kuwa maafisa kadhaa wa polisi walikiri kuwa kikosi maalum cha usakama kilihusika na kutoweka na hatimaye mauaji ya washukiwa wa ugaidi, hasa viongozi wa dini ya kiislamu waliokisiwa kuwa na siasa za misimamo mikali.

Lakini Katibu wa Wizara ya Habari nchini Kenya amesema ripoti hiyo haina msingi wowote na kutaka shirika hilo la habari kuiomba msamaha.

Ni ahadi yetu kuhakikisha unapata taarifa zote zinazotokea ulimwenguni, hivyo ni vyema ukaendelea kuwa nasi kila iitwapo leo nasi tunaahidi kuendelea kukuhabarisha.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname