UMILIKI WA WIMBO WASABABISHA MSANII KUCHAPWA NGUMI



Imeelezwa kuwa rapper Drake ameingia katika bifu baada ya kushikana mashati na mwanamziki Puff Daddy nje ya klabu mmoja huko Miami siku ya Jumatatu ya Novemba 24.

Kwa mujibu wa mtandao wa "Page Six" umeripoti kuwa ugomvi huo ulitokea kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya DJ Khaled kwenye klub ya LIV iliyopo kwenye hoteli ya Fontainebleau.

Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa bifu hiyo inahusishwa na haki za wimbo ambao unamuhusu Drake na Puff Daddy ambao hadi sasa haujafahamika ni wimbo upi na endapo kama umeshatoka au laa!


Puff Daddy
Msanii Drake

Mbali na hayo mtandao wa Tmz umeripoti kuwa Diddy alisema “You will never disrespect me” kabla ya kufanya maamuzi yake ya kurusha ngumi kwa Drake, jambo ambalo lilimshangaza Drake.

Dj wa Rick Ross ‘DJ Sam Sneaker‘ alibainisha kuwa Drake aliumia sana bega na kusababishwa kupelekwa hospitalini.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname