HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MSANII WA BONGO MOVIE KUHUSU KUKAA LEADERS CLUB



Mwigizaji mkongwe kwenye filamu Bongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amesema kwamba anajutia maisha aliyokuwa akiishi kipindi alipokuwa ‘Bongo Movie Unity’ kwani alipoteza muelekeo kutokana na ile kasumba ya kukaa Viwanja vya Leaders kila kukicha kwa mambo yasiyokuwa na tija.

Akizungumza na waandishi wa GPL hivi karibuni, Cathy, alisema kati ya vitu vinavyomuumiza ni kupoteza fedha nyingi kwenye vikao vya Leaders bila kuingiza fedha yoyote na sasa anajuta.

“Unajua sisi Wapare tumekuja mjini kutafuta hela sasa mimi nilikuwa natoa tu bila faida yoyote. Nilikuwa natumia pesa kununua mafuta ya gari kuendea pale, kununulia vinywaji na matumizi mengine lakini manufaa sijayaona."

Hata hivyo Cathy alisema kwamba anamshukuru Mungu kwa sababu amemtoa kwenye hilo kundi na sasa anafanya kazi zake.

Sasa nafanya kazi zangu za maana zaidi na ile tabia ya kukaa na kunywa au kutumia fedha kijinga haipo tena,” alisema Cathy.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname