SAKATA LA ESCROW LAMPONZA PROFESA TIBAIJUKA



Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo  Makazi Profesa Anna Tibaijuka
Baada ya Watanzania kusuburi kwa muda mrefu kuhusu ni nini angeamua Mh Rais Dr Jakaya Kikwete kuhusu lile sakata la Escrow hatimaye Disemba 22 Rais Kikwete ameamua kumuachisha kazi Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo Makazi Profesa Anna Tibaijuka kutokana na tuhuma za kupata mgao wa Fedha za Akaunti ya Escrow kiasi cha bilioni Moja na Milioni Mia Sita ambazo alidai amepewa mchango kwa ajili ya shule.

Rais Jakaya amesema kwamba “tumeamua mwenzetu huyu atupishe ili tuchague mtu mwingine wa kuhudumu katika wizara hiyo kutokana na maswali magumu”
Rais Kikwete katikati akisisitiza jambo alipokuwa akilihutubia Taifa kupitia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee
Aidha, Rais Kikwete aliongeza kuwa Profesa Tibaijuka akiwa kama Mtumishi wa serikali ambaye anatakiwa kufuata maadili ya Utumishi wa umma aliamua kupokea kiasi kikubwa cha fedha huku akijua kimaadili kama mtumishi wa serikali haitakiwi.

Uamuzi huo wa Rais Dr. Jakaya Kikwete ameutoa alipokuwa akizungumza na taifa kupitia Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Mbali na Profesa Tibaijuka kuachishwa kazi kwa upande wa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eliackhim Maswi Rais amesema ameagiza uchunguzi ufanyike katika muda wa siku mbili au tatu hivi atapewa taarifa ya uchunguzi huo na kuchukua hatua stahiki.

Sambamba na hayo pia kwa upande wa Majaji wa Mahakama Kuu waliotuhumiwa Rais Kikwete amesema anamwachia Jaji Mkuu Mh. Jaji Mohammed Chande Othman ili achukue hatua za kimaadili kutokana na taratibu za kimahakama na mara baada ya kujiridhisha atapewa taarifa na Jaji Mkuu na kuchukua hatua pia.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname