MISS WORLD SASA WAAMUA KUONDOA KIPENGELE CHA VAZI LA UFUKWENI



 
Miss World 2014 Rolene Strauss ambaye ni mrembo wa Afrika Kusini
Shindano la ulimwende duniani maarufu kama Miss World sasa halitakuwa likihusisha kipengele cha warembo kuvaa nguo za ufukweni (kuogelea)

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa shindano hilo Chris Wilmer, ambaye amesema kuwa, sababu ya kfutwa kwa kipengele cha mashindano ya nguo za kuogelea ni kutokana na kushindwa kuendana na vipengele vingine vya mashindano hayo.

Mbali na hayo, Mkurugenzi huyo amesema kuwa mashindano hayo pamoja na kuwa mashindano ya urembo, lakini hayahusishi urembo pekee bali urembo na sababu maalum na hakukuwa na sababu yoyote maalum ya kujumuisha kipengele cha nguo za kuogelea .

Aidha, Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kwamba Mshindi wa Miss World anapaswa kuwa balozi na msemaji wa jamii ya watu sio malkia wa urembo pekee. Huku akiongeza kuwa maadili na kile anachowakilisha mshindi wa Miss World ndio kinachotazamwa kwa mshindi hivyo kwa sababu hiyo Miss World haitakuwa na kipengele cha shindano la nguo ya kuogelea.

Itakumbukwa kwamba kipengele hiki kimekuwepo tangu mwaka 2001 wakati kilipopewa jina la Beach Fashion, huku kikifanywa kama kipengele binafsi ndani ya shindano hilo.

Ni haki yako kupata habari zote kutoka kwetu, tafadhali endelea kutuunga mkono msomaji wetu.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname