MWANAUME AHANGAIKA NA UREMBO ILI AFANANE NA KIM KARDASHIAN


Kijana Jordan James mwenye hamasa ya kuwa kama Kima Kardashian



Kijana Jordan James kutoka nchini Uingereza mwenye umri wa miaka 23 ambaye amekuwa na shahuku kubwa ya kutaka kufanana na mwanadada ambaye hutajwa mara kwa mara vinywani mwa watu wengi duniani yaani Kim Kardashian.

Jordani James katika kutimiza shahuku yake hiyo ya kufanana na Kim Kardashian amefanya mambo ya ajabu akijitahidi kufanana na Kim kwa kujiongeza urmbo bandia, hasa kufanya midomo yake kuwa mikubwa akitaka ifanane na ya Kim.

Inaelezwa kuwa kijana huyo ametumia kiwango cha pesa Pauni 150,000 au dola laki mbili na arobaini katika harakati zake za kutaka kufanana kama Kim, huku ikielezwa kwamba pesa hizo zote amezitumia kwa kufanyiwa upasuaji na kuongezwa urembo bandia.

Kijana Jordan James aliliambia jarida la The Sun kwamba alianza kumuenzi Kim Kardashian mwenye umri wa miaka 33 baada ya kutazama makala ya kipindi kijulikanacho kama ''Keeping Up With The Kardashians.'' Kipindi kinachohusu Kim na Familia yake.

“Ninapenda kila kitu kumhusu Kim, yeye ndiye mwanamke mrembo zaidi duniani. Ngozi yake ni nyororo, nywele zake zinapendeza yaani kila kitu kumhusu kinanipendeza” alisema Jordan James akiliambia jarida la The Sun.'
Kijana Jordan James mwenye shahuku ya kutaka kuwa kama Kim Kardashian
Jordan amefanyiwa upasuaji kuongeza urembo bandia zaidi ya mara 50 katika juhudi zake za kutaka kufanana kama Kim, amerembeshwa midomo, ametolewa nywele kwa kutumia miale ya Laser, amewekwa Tatoo na hata kubadilisha kope zake na mengine mengi. Lakini mabadiliko hayo yote yamemgeuza sura sana Jordan na kumfanya kuwa kichekesho kwa watu wengi.
Kim Kardashian
''Mimi mwenyewe hucheka watu wanapojaribu kunitusi au kunikejeli, na kuniambia kwamba mimi ni kama plastiki tu, yaani kila kitu mwilini mwangu ni baandia. Lakini hilo hainijalishi.'' alisema Jordan James



1 comment:

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname