HUYU NDIYE MSANII WA BONGO MOVIE AMBAYE AMEAMUA KUBADILISHA JINA LAKE



Star wa Bongo Movie, Rose Ndauka amesema kwamba kuanzia sasa jina lake jipya litakuwa ni “Bakita”

Star huyo ambaye kwa sasa yupo katika utengenezaji wa filamu mpya ambayo inafanyika chini ya kampuni ya Bulls Entertainment, aliandika mtandaoni kwa kifupi kuwa jina lake jipya ni Bakita.“My new name it's Bakita#new”

Aidha, suala hilo limeonekana kuwaacha na maswali mashabiki wengi, huku wakijiuliza nini hasa kimemfanya awe na jina jipya msanii huyo.

Mbali na hayo Rose Ndauka hivi karibuni alionekana akiwa Location na mwigizaji na muongozaji wa filamu Richie, na kuahidi kazi mpya na kali inafanyika na hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula.

Tunasema asante kwa kufanya maamuzi sahihi ya kutembelea habarimkusanyiko.blogspot.com, tafadhali tunaomba uendelee kuwa nasi siku zote kwa habari zaidi katika nyanja zote.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname