ZAIDI YA WATU 100 WANAHOFIWA KUFA MAJI DRC



Ripoti kutoka Jamhuri ya Demokrasi ya Kongo zinaeleza kuwa watu zaidi ya 100 wanahofiwa kufariki dunia katika ajali ya feri.

Taarifa zinasema kwamba jahazi iliyojaa abiria imezama katika Ziwa Tanganyika kusini-mashariki mwa nchi siku ya Alhamisi.

Waziri wa usafiri wa jimbo hilo la Katanga, Laurent Sumba Kahozi), aliliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa miili kama 129 imeshapatikana

Hata hivyo, inaarifiwa kuwa watu 232 walinusurika katika ajali hiyo ajali ilyoitokea Alhamisi usiku kaskazini mwa jimbo la Katanga baina ya miji ya Moba na Kalemie.

Pamoja na hayo, waandishi wa habari wanasema ajali kama hizo zinatokea kawaida kwa sababu feri mara nyingi zinakuwa zimejaa mno.

Habarimkusanyiko.blogspot.com inashukuru kwa kutuunga mkono.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname