KAMA UNGEPENDA KUJUA KUHUSU MAANDALIZI YA TAMASHA LA KRISMASI NI VIZURI UKASOMA HAPA

Kampuni ya Msama Video Productions imesema kwamba mwaka huu wamejiandaa vizuri kufikisha ujumbe wa neno la Mungu katika Tamasha la Krismas kutokana na kuwa na vifaa vipya na vya kisasa vyenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi katika mazingira yoyote.

Akizungumza na Dira ya Mtanzania, Meneja wa kitengo hicho, Alpha Kigalla ameeleza sababu za kufanikisha katika tamasha hilo ni kwa sababu ya umahiri wa watendaji wa kitengo hicho na ndio chachu itakayofanikisha kutekeleza ibada hiyo kwa waumini na mashabiki watakaojitokeza katika Tamasha hilo.

Aidha, Kigalla alitoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kujitokeza kwa wingi kushuhudia kazi za kitengo hicho kilicho katika kampuni ya Msama kwani kwa sasa wana vifaa vya kisasa zaidi.

“Msama Video Productions ina vifaa vipya na vya kisasa zaidi na hata watendaji wake wako makini zaidi na utekelezaji wa kazi zao, hivyo wadau wa muziki nchini kujitokeza kufanikisha kazi zao,” alisema Kigalla.

Mbali na hayo, Meneja huyo aliwataka wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kujiandaa na kazi bora za Msama Video Productions ambazo zitafanikishwa kupitia waimbaji mbalimbali wa muziki huo.

 Asante kwa kuendelea kutembelea habarimkusanyiko.blogspot.com, tafadhali endelea kutuunga mkono

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname