KUELEKEA KUHITIMISHA MWAKA 2014, HIKI NDICHO ALICHOKISEMA ZAMARADI MKETEMA


Zamaradi Mketema

Mtangazaji wa kituo cha luninga cha Clouds Tv Zamaradi Mketeama kutoka kipindi cha Take One, ameamua kusema haya yafuatayo katika kuelekea mwaka 2015, ni vizuri ukasoma pengine unaweza kujifunza kitu kupitia haya aliyonena mtangazaji huyu.

"...Kila mtu utaskia NEW ME.. Leaving behind this and that lakini tusidanganyane ama niseme usijidanganye... WEWE ni YULE YULE kinachobadilika ni herufi tu.. inatoka 4 inaingia 5.. lakini mipango yako ni ile ile.. TABIA ZAKO ni zile zile, maisha yako ni yale yale.. wanaokuzunguka ni wale wale na hata ndoto zako ni zile zile... NOTHING SPECIAL!!! Na kama kila kitu ni KILE KILE basi hata WEWE utabaki YULEYULE sababu vinavyoendesha maisha yako vyote ni VILEVILE!!! Hayo mabadiliko unayosema yatatokea wapi!! MWAKA MPYA hauji na zawadi ya MABADILIKO kama wewe binafsi hutaki kubadilika.. na ukiamua MWAKA MPYA wa mabadiliko unaweza hata ukawa mwezi wowote katika mwaka.. JIULIZE MWAKA JANA wakati unaingia hukuzungumza hayahaya!!??? ULIFANYA NINI!!?? Mambo ya MWAKA MPYA MAMBO MAPYA ni maneno tu yanapatikana popote...TUUFURAHIE TU ukiingia na kumshukuru MUNGU basi lakini mambo ya NIMEKUWA MTU MPYA utayahakikisha mwenyewe ukifika mwezi february baada ya kujigundua huna ulichobadilika.. usisubiri mwaka upinduke ndio ujiongeleshe kuhusu kubadilika, KILA SIKU ni siku ya mabadiliko..... NAWAOMBEA KHERI WOTE WENYE MABADILIKO YA UKWELI WAFANIKISHE na wale wenye longolongo za insta kila mwaka mpya pia kila la kheri huenda ikakusaidia pia maana PRACTISE MAKES PERFECT!!!

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname