MASHINDANO YA MISS TANZANIA YAFUNGWA, YADAIWA KUWAPO NA UPENDELEO PAMOJA NA RUSHWA



 Mashindano ya ulimwende hapa nchini maarufu kama Miss Tanzania yamefungwa kwa miaka miwili kutokana na waandaaji kudaiwa kukiuka taratibu na kanuni za uendeshaji.

Mashindano hayo yaliyofunguliwa mnamo mwaka 1994 yamekuwa yakidaiwa kuwa na upendeleo pamoja na kuhusishwa na rushwa ndani yake kulingana na malalamishi ambayo yamekuwa yakitolewa na wananchi pamoja na washiriki.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Tanzania Basata, Godfrey Mngereza, amesema kwamba kamati ya miss Tanzania ilikiuka kanuni na taratibu zinazoongoza mashindano hayo.

"Ni kweli kwamba tumeifungia Miss Tanzania kwa miaka miwili, lakini haya si maazimio ya tathmini iliyofanyika mapema mwezi huu, bali kulikuwa na vikao mbalimbali vilivyofanyika na si kimoja, ni uamuzi mgumu ambao umekuja kutokana na sababu maalum,"

Aidha, imedaiwa kuwa mashindano yaliyofanyika Disemba 12, mwaka huu hayakufikia uamuzi, bali vikao mbalimbali vilivyoendeshwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Basata ndivyo vilivyofikia hatua hiyo ili kutoa nafasi kwa waandaalizi kujipanga upya.

Baadhi ya maswala yaliyoibuka ni pamoja na baadhi ya warembo walidaiwa kutumiwa kingono.Vilevile hakuna utaratibu wa kuwasajili warembo hao uliofuatwa kuanzia vitongojini hadi kufikia fainali.

Sambamba na hayo, Mngereza alisema baraza limegundua kuwa baadhi ya washiriki walichaguliwa kwa upendeleo bila ya kuwa na sifa zilizohitajika

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname