NDEGE YAPOTELEA HEWANI, YADAIWA HUENDA ILIISHIWA MAFUTA

Shirika la ndege la AirAsia limesema kuwa limeanzisha shughuli ya kuitafuta ndege yake iliyopoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege dakika 45 baada ya kuondoka kwenye mji wa Surabaya nchini Indonesia.

Taarifa zinaarifu kuwa zaidi ya watu 160 walikuwamo ndani ya ndege hiyo ya Airbus 320 iliyokuwa safarini kwenda nchini Singapore.

Habari za zinaendelea kusema kwamba wengi wa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo walikuwa wakitokea nchini Indonesia.

Aidha, msemaji wa Wizara ya Usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya Kalimantan na Java. Huku wataalam wa safari za ndege wakisema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname