WAFANYAKAZI WA SEKTA YA MADINI WASHAURIWA KUJIUNGA NA TAMICO



Mwanza, Na Goodluck Ngowi

Wafanyakazi katika sekta za ujenzi, nishati na migodi wameshauriwa kujiunga na matawi ya Chama cha Wafanyakazi wa Migodi, Nishati, Ujenzi na Kazi nyingine (TAMICO) kwa lengo la kuweza kupata haki zao za msingi ikiwemo mikataba inayokidhi matakwa ya kisheria.

Wito huo umetolewa jana jijini Mwanza na Katibu wa TAMICO Kanda ya ziwa, Joseph Mang'ana, ambaye alisema licha ya kuwepo kwa wafanyakazi wengi katika sekta hizo ni wafanyakai 1,495 pekee ndio waliojiandikisha katika chama hicho.

"Kwa mujibu wa takwimu tulizonazo kuna wafanyakazi wasiopungua 5,000 katika sekta hizi za nishati, madini na migodi lakini ni idadi ndogo waliojiandikisha, hali inayowakosesha faida mbalimbali kama mafunzo ya haki zao za msingi, kutetewa na wanasheria na mawakili wetu pindi wanapoachishwa kazi na kunyanyaswa na waajiriwa wao" alisema Mang’ana.

Aidha, Mang'ana aliwashauri waajiri hasa wa makampuni ya ujenzi kuhakikisha wanawapa wafanyakazi wao mikataba ya kudumu na kuweka mazingira bora ya kazi kwa wafanyakazi hao kama inavyoelekezwa na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazinini.

Mbali na hayo, Mang'ana alisema faida nyingine za kujiunga na TAMICO ni kupata haki ya kuchagua viongozi na kuchaguliwa kama wawakilishi wa chama hicho katika matawi maeneo yao ya kazi.

Asante kwa kuendelea kuifanya habarimkusanyiko.blogspot.com kuwa sehemu yako ya kupata habari  tafadhali endelea kuwa nasi na tunadhamini sana uwepo wako kwetu.


No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname