Ronaldo ametwaa tuzo hiyo kwa kuwashinda wapinzani wake Lionel Messi na Kipa Manuel Neuer kwa asilimia 37.66 ya kura zote, huku Lionel Messi akipata asilimia 15.76% na Manuel Neuer mwenye asilimia 15.72%.
Ronaldo, ambaye ni raia wa Ureno ametwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo, lakini ni mara yake ya tatu kwa kuwa mara ya kwanza aliibeba 2008 akiwa na Manchester United.
Itakumbukwa kwamba mwaka jana, Ronaldo akiwa na timu ya Real Madrid aliiwezesha kutwaa ubingwa wa Ulaya, Copa del Rey, Uefa Super Cup, pia ubingwa wa dunia, ambao yeye kwa wakati huo alifunga mabao 56 katika mechi 51.
Baadhi ya picha za matukio katika utoaji wa tuzo hizo
Wengine waliopata tuzo pia ni pamoja na James Rodriguez aliyepata tuzo ya goli bora na katika tuzo ya mwanasoka wa kike ameshinda Nedine Kassler, huku tuzo ya mlinda mlango bora akishinda Manuel Neur, lakini kwa upande wa tuzo ya kocha bora imeshikiliwa na Mjerumani Joachim Law
No comments:
Post a Comment