SERIKALI YAPANIA KUPAMBANA NA VITENDO VYA MAUAJI KWA WALEMAVU WA NGOZI



Serikali imeunda kikosi maalum kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi –Albino- na kupiga marufuku kuanzia wapiga ramli wote ambao wanaelezwa kuchangia mauaji ya watu hao.

Akizungumza na wanahabari Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe Ameitaja mikoa inayotarajiwa kuanza kwa operesheni maalum ya kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya walemavu katika juhudi za kukomesha matukio hayo, ambayo yameelezwa kuanza kuibuka tena.

Operesheni hiyo maalum itaanza na mkoa wa Mwanza, Simiyu, Geita, Tabora na Shinyanga, huku operesheni hiyo ikitarajiwa kuendelea katika mikoa mingine.

Aidha, Waziri Chikawe amesema operesheni hiyo itaanza baada ya wiki mbili kwa ushirikiano wa polisi na wawakilishi kutoka chama cha watu wenye ulemavu Tanzania.

Akielezea kazi ya kikosi hicho maalum waziri Chikawe amesema ni kupitia pia kesi zote zilizowahi kufikishwa mahakamani kuhusiana na vitendo hivyo.

Kuhusu wapiga ramli waziri alisema jeshi la Polisi litaandaa operesheni maalum kuwatafuta na kuwashika wapiga ramli nchi nzima na kuwashtaki. Huku akiongeza kuwa wapiga ramli hao wanajulikana na wananchi hivyo anawaomba wananchi kusaidia kuwatambua.

Mbali na hayo, waziri ameyataka madhehebu ya dini mbalimbali na mashirika ya kijamii kutoa elimu juu ya jambo hilo. Huku sababu kubwa iliyotajwa inayosababisha watu kutafuta viungo hivyo vya binadamu inaelezwa kuwa ni kupata utajiri.
Asante kwa kuendelea kuwa nasi katika kupashana habari, tafadhali endelea kutembelea habarimkusanyiko.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname